Pages

Saturday, 19 October 2013

MBEYA KUNANI? AUAWA KWA KUKATWA KICHWA NA MAITI YAKE KUTUPWA KARIBU NA NYUMBANI KWAKE!!

Baadhi ya majirani wakiwa jirani na mwili wa marehemu Seba wakisubiri polisi kuja kuuchukua mwili huo


Mwili wa Marehemu Seba ukiwa umefunikwa.





 
SEBA ERNEST MWAKASULA[45] ameuawa  kwa kukatwa kichwani na  tumboni na vitu vyenye ncha kali  na mtu au watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa mita chache kutoka nyumbani kwake.

Mke wa marehemu JOYCE DANIEL[39]amesema waliagana na marehemu majira saa mbili usiku akimtaarifu kuwa asubuhi ya octoba 19 mwaka huu atasafiri kuelekea Wilaya ya CHUNYA kwa ajili ya kujenga makaburi.

Aidha imedaiwa baada ya kutoka nyumbani mdogo wa marehemu alipita kilabuni ambapo watu kadhaa walimwona marehemu akipata viburudisho.


Baadhi ya majirani wamesema kuwa hawakusikia sauti yoyote ya mtu kuomba msaada ingawa ni karibu na makazi ya watu hali inayosadikika mauaji kufanywa eneo jingine na mwili kutupwa karibu na nyumbani kwake


Mwenyekiti wa kijiji cha NSONYANGA ASUMILE MTAWA amesema alipata taarifa kutoka kwa mtendaji wa kijiji ambapo walifika eneo la tukio na kukuta marehemu amekatwa kichwani na utumbo ukiwa nje.



Diwani wa kata ya Mahongole BROWN MWAKIBETE amesema kuwa kitendo kilichofanywa na wauaji hao ni cha kinyama ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi li watuhumiwa wakamatwe ili kujibu tuhuma za mauaji.



Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Daktari kisha kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa mazishi.



Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kutoa wito kwa mtu au watu wanaowafahamu wliohusika na tukio hilo watoe taarifa polisi il wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.



Picha na Ezekiel Kamanga

Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment