VILIO vilitawala juzi Jumanne wakati nguli katika utangazaji Bongo, Julius Nyaisangah ‘Uncle J’ akiagwa, lakini wengi walionekana kumlilia zaidi swahiba wake wa karibu, Charles Hillary ‘Chalz Hillary’.
Jopo la waandishi wetu lililofika mapema katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar katika Ibada ya kumuaga marehemu, lilishuhudia mijadala ikiendelea katika makundi kuhusu upweke alioachwa nao Hillary.
Kwa sasa Hillary ni mtangazaji katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) lenye makao yake makuu, jijini London.
Mwandishi mmoja mwandamizi aliyekataa jina lake kutajwa, alisikika akisema; “Nilimsikia Charles Hillary akihojiwa BBC, alilia sana, akasema lazima aje amzike rafiki yake, lakini mpaka sasa sijamuona. Masikini, kama namuona vile, atakuwa na hali mbaya.”
Mwingine alisema: “Inawezekana amechelewa ndege lakini kama atafanikiwa kuja, anaweza kukodisha ndege ndogo ikamuwahisha Tarime kwenye mazishi, maana anazikwa kesho (jana).”
HESHIMA
Watangazaji na wadau wa habari nchini waliofika viwanjani hapo waliipongeza serikali kwa heshima kubwa waliyompa marehemu Nyaisangah kwa kuomba shughuli za kuagwa kwa mwili wake ifanyike pia Dar es Salaam, ambako alikuwa na marafiki wengi.
Mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais, Dk. Ali Gharib Bilal ambaye alitoa salamu zake za rambirambi na kuwataka wanafamilia na wanahabari wote kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
VINGOZI WENGINE
Mbali na Dk. Bilal, vingozi wengine waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa taifa we Chadema, Freeman Mbowe, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa na viongozi wengine.
Mbali na hao, Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) Dk. Reginald Mengi, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, John Kitime ambaye aliwawakisha wanamuziki wote na Mkurugenzi wa Aset, Asha Baraka.
GPL.
No comments:
Post a Comment