Pages

Sunday, 20 October 2013

KANISA LAGOMA KUMZIKA MCHUMBA WA UFOO SARO....LADAI KIFO CHAKE KINA UTATA..!!




Familia ya Anthery Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi Jumapili iliyopita baada ya kumuua kwa risasi mkwewe, Anastazia Saro, amezikwa bila huduma ya kikanisa kijijini kwao Ongoma.

Kanisa Katoliki, Parokia ya Uru ilishindwa kutoa huduma hiyo kutokana na mazingira ya kifo chake.

Licha ya hali hiyo kujitokeza, familia hiyo, ilionyesha nia yake ya kwenda kumuangukia Paroko wa Parokia wa Kanisa hilo, ili aridhie familia ya Anthery, isome misa maalumu ya kuomba ndugu yao afutiwe dhambi inayomkabili.

Mushi (40), alijipiga risasi baada ya kumuua mkwewe na kumjeruhi mzazi mwenziwe Ufoo Saro, mtanzangazi wa kituo cha televisheni cha ITV,  eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Wakati familia ya Mushi ikiazimia hilo, kiongozi aliyeteuliwa na familia kufanya ibada ya maziko, baba mdogo wa Mushi, Ugolin Mushi alisema kuwa Watanzania wanapaswa kutomhukumu kwa alichokitenda na kwamba imetosha kwa kuwa kinachoelezwa kila kona ya nchi baada ya tukio hilo ni sawa na mbu kubadilika na kuwa tembo.

“Sisi ni nani hadi tumhoji Mwenyezi Mungu juu ya kilichotokea maana mbu anaweza kubadilika na kuwa mkubwa kama tembo kutokana na habari zinazotangazwa.


"Anayejua ukweli huu ni Anthery na Mungu wake…Lakini Mungu amsamehe makosa yake wakati wa vita na wakati wa amani, wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa na akafurahi na malaika huko aendako,” alisema.

Hata hivyo, mtoto wa marehemu, Alvin Anthery, ambaye amezaa na Ufoo, hakuweza kumzika baba yake kutokana na sababu zisizojulikana.

Hali ilikuwa tulivu nyumbani kwa marehemu Kijiji cha Ongoma, Uru Kaskazini, tofauti na matarajio ya wengi baada ya kuwasili kwa mwili huo usiku wa kuamkia jana, ingawa mamia ya wakazi wa Uru walifurika kushuhudia mazishi ya Anthery ambaye  amelitikisa taifa kwa siku kadhaa kutokana na tukio la mauaji Oktoba 13, kugonga vichwa vya habari.

Juzi, familia ya Anthery, ilinukuliwa wakati wa kuuaga mwili wake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), ikiliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kutokana na ndugu yao kukutwa na risasi mbili.

Mwili wake baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ulikutwa na risasi mbili, moja ikiwa kwenye ubongo na nyingine kwenye jeraha lililo pembeni ya sikio.

Licha ya kanisa kutotoa huduma ya ibada ya mazishi ya Anthery, watawa wa kanisa waliohudhuria katika msiba huo walishindwa kuendesha ibada kutokana na taratibu

No comments:

Post a Comment