Pages

Tuesday, 22 October 2013

KAMPUNI YA FEDHA INVESTMENT YATOA MSAADA KWA KITUO CHA KULEA WATOTO YATIMA, KIBAHA


Uongozi wa Kampuni ya Fedha Investment ya Jijini Dar es Salaam,ukiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Kibaha (Kibaha Children's Village Centre),ambacho kipo chini ya Taasisi ya The EOTF Orpham Centre,inayoongozwa na Mama Anne Mkapa,mara baada ya kukabidhi msaada wao wa Sh. Milioni 1 kwenye kituo hicho,kilichopo katika kijiji cha Mwendapole,Kibaha Mkoani Pwani.
Wakurugenzi wa Kampuni ya Fedha Investment,Esta Maro (kushoto) na Devota Mtambo (pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya The EOTF Orpham Centre,Mama Anne Mkapa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watoto wa Kituo cha Kibaha Children's Village Centre.Aliesimama kushoto ni Dada Sia Tito.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fedha Investment, Devota Mtambo (kushoto) akikabidhi hundi ya sh. Mil. 1 kwa Meneja wa Kituo hicho,Bw. Deogratius Mosha (aliembeba mtoto) ikiwa ni sehemu ya msaada walioutoa kwa kituo hicho.
Mwenyekiti wa Taasisi ya The EOTF Orpham Centre,Mama Anne Mkapa akishumuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Fedha Investment, Devota Mtambo baada ya kukabidhi msaada wake kwa Kituo cha Kibaha Children's Village Centre.
Watoto wa Kituo cha Kibaha Children's Village Centre wakitoa burudani kwa Wageni wao.
 
Mmoja wa Watoto wa Kituo hicho,aitwae Ester akimalizia kazi aliyopemwa na Mwalimu wake.
Watoto wakiwa kwenye Ibada baada ya Kutoka Shule.
Meneja wa Kituo cha Kibaha Children's Village Centre,Deogratius Mosha akionyesha Ramani ya eneo la Kituo hicho kwa Wageni wake.
Meneja wa Kituo cha Kibaha Children's Village Centre,Deogratius Mosha (kushoto) akifafanua jambo mbele ya wageni wake waliofika kwenye Kituo hicho.
Wakitembelea maeneo mbali mbali ya Kituo hicho.
 
Meneja wa Kituo cha Kibaha Children's Village Centre,Deogratius Mosha akiwaonyesha wageni wake namna kituo chao hicho kilivyoweza kupanda matunda aina ya Mananasi.
Bwala la kufugia Samaki.
Mandhali ya Kituo hicho.
Mwenyekiti wa Taasisi ya The EOTF Orpham Centre,Mama Anne Mkapa akifurahi na Watoto wa Kituo hicho.

No comments:

Post a Comment