Habari tulizozipata ni kwamba Jamal emil Malinzi
amefanikiwa kushinda uchaguzi wa TFF kwa nafasi ya urais aliyokuwa
anagombea dhidi ya Makamu wa zamani wa Rais wa TFF Athumani Nyamlani.
Uchaguzi huo, uliotawaliwa na kashkashi za hapa na pale, ulifanyika katika ukumbi wa NSSF WATER FRONT, Dar es salaam
Jamal Malinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa
Kagera ameshinda uchaguzi huo ikiwa ni mara yake ya pili kugombea baada
ya kushindwa na Rais wa zamani wa TFF Leodgar Chillah tenga mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment