Wednesday, 23 October 2013

HIVI KWELI MNAUWA KISA KAIBA KUKU WATATU EEH MUNGU BABA!!.......

MAAJABU MBEYA; KUKU ATAGA YAI PEMBENI YA KABURI

 
Ndugu wa marehemu Frank Shoka aliyetuhumiwa kwa wizi wa kuku mwili wake ukisubiriwa kuja kuchukuliwa napolisi
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula aliyesimama kushoto amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.
Hata hivyo katika  hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.
Polisi wakiuchukuwa mwili wa marehemu Frank

WAKATI jeshi la polisi Mkoani Mbeya likijitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, bado hali imezidi kushamiri baada  watu wawili kuuawa kwa tuhuma za wizi wa mifugo.

Matukio hayo ywmetokea katika Wilaya za Kyela na Mbeya vijiji yakiwemo ya wizi wa kuku na ng’ombe jambo lililopelekea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua bila kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.

Katika Tukio la kwanza lililotokea katika kitongoji cha Katusi kijiji cha Mjere wilaya ya Mbeya vijijini wananchi wamemuua Frank William Shoka(30) kwa tuhuma za wizi wa kuku watatu mali ya Dismas Rashid(41)mkazi wa kijiji hicho.

Akizungumzia tukio hilo, Dismas Rashidi aliyeibiwa kuku hao  alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 20,mwaka huu na kuongeza kuwa marehemu alivunja banda la kuku majira ya usiku wa manane na kuchukua kuku watatu wakati yeye akiwa amekwenda kumuuguza mwanae katika kituo cha Afya Mjere ambako aliandikiwa sindano za masaa.

Alisema Baada ya kurudi nyumbani na kukuta kuku wake hawapo alianza kufuatilia na kumkuta marehemu akiwa na kuku hao katika kituo cha mabasi akitaka kuwasafirisha kwenda Mbeya,alipoulizwa juu ya kuku hao alikosa majibu wakati huo ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri.

Alisema mtuhumiwa huyo  baada ya kushindwa kutolea maelezo juu ya kuku hao wananchi walianza kumpiga kwa kutumia fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyomfanya kupoteza maisha papo hapo mita chache kabla ya kufikishwa katika ofisi ya kijiji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.
Hata hivyo katika  hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!