Pages

Sunday, 20 October 2013

HAKIKA HAPA DUNIANI TWAPITA" MANENO YA MTANGAZAJI MKONGWE ABOUBAKAR LIONGO JUU YA KIFO CHA JULIUS NYAISANGA...(UNCLE J)..


Uncle J Julius Nyaisanga Omang'ere umeondoka kaka huku bado tasnia hii ikiwa yakuhitaji sana.Ni wewe uliyonichukua ukiwa pamoja na Charles Hillary kwenda kuanzisha Radio One,ukaenda kwa marehemu baba yangu Mzee Liongo kumuhakikishia us alama wangu katika chombo hicho Cha kwanza binafsi.Ni mengi sana haya tosha hapa kuyaandika.Nilikuja Morogoro ukanipa makaribisho makubwa, ambayo kwa hakika nilidhani sistahiki kuyapata, lakini kwa tabia yako ya upendo ulinipa,Uncle J Sauti yako laini, matamshi mazuri ya uhakika na uwezo mkubwa wa kuzungumza na msikilizaji, vitakuwa Hazina kubwa kwa wale watakaotaka kupiga hatua kiutangazaji,mioyo yetu inabubujikwa na damu kukulilia.Hakika Hapa duniani twapita iko siku tuaonana huko ulikoenda, wasalimie, Karim Besta,Hassan Mkumba, Nadhir Mayoka, Iddie Mchatta, Tumbo Risasi,Khalid Ponera, David Wakati na ma comrade wengine waliyotangulia


No comments:

Post a Comment