Thursday, 24 October 2013

WAZIRI MKUU PINDA AENDELEA NA ZIARA NCHINI GUANZHOU- CHINA




WAKATI HUOHUO TAARIFA NYINGINE ZINATUHABARISHA KUWA

SERIKALI ya Tanzania leo imeingia mikataba saba na makampuni sita ya Kichina yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.7 (Sh. trilioni 2.72) ambazo zitawekezwa kwenye ujenzi wa miradi ya umeme na nyumba za makazi na biashara.
Makubaliano ya uwekezaji huo mkubwa yameshuhudiwa leo (Alhamisi, Oktoba 24, 2013)  na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mawaziri wengine wa Serikali baada ya kusainiwa kwa mikataba saba ya uwekezaji katika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa nchi.
Utiaji saini huo ulifanywa mara baada ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano la Uwekezaji na Biashara kati ya Tanzania na China (Tanzania China Business Forum) uliofanyika kwenye hoteli ya Dong Fang, jijini Guangzhou jimboni Guangdong, China. Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Baraza la Biashara la China Afrika (China Africa Business Council-CABC) linashirikisha wafanyabiashara wa China na Tanzania.
Mikataba iliyosainiwa leo ni kati ya Shirika la Umeme (Tanesco) na Kampuni ya Tabiau Electric Apparatus Stock Co Ltd (TBEA) ambao ni kwa ajili ya ujenzi wa njia ya umeme ya msongo mkubwa wa 400kV katika Gridi ya Taifa inayotoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini Mashariki hadi Arusha.
Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO, Bw. Felchesmi Mramba ndiye aliyesaini mkataba huo wenye thamani ya dola za marekani milioni 692.7. Bw. Mramba pia alisaini mkataba mwingine na kampuni ya Shanghai Electric Power ambayo ndio itajenga mtambo wa Kinyerezi III.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!