Pages

Tuesday, 29 October 2013

BABA MZAZI ATUMIA SIRAHA ZA ULINZI KUMWADHIBU MTOTO WAKE WA MIAKA 10 KWA KOSA LA KUTOKWENDA SHULE JIJINI MBEYA






Victoria Mukama (10) akiwa hospitali ya rufaa mbeya baada ya kupigwa na baba yake mzazi  sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa  vya ulinzi likiwemo Lungu.
 Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

 
Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.
 
 majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.
 
Victoria Mukama (10) baada ya matibabu
 KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar Mukama  mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.
Kwa mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Alisema mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo kwa mwanaye.

Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.

Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa kasha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya matibabu.

Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.

No comments:

Post a Comment