Sunday, 4 December 2016

Serikali yatoa trilioni moja za kununua dawa

[​IMG]

AHADI ya serikali ya kuanza kusambaza dawa katika hospitali zote nchini kutokana na madai ya kuwepo kwa uhaba wa dawa za aina mbalimbali, imeanza kutekelezwa.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani mkoani Arusha amesema Serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa na kuhakikisha pia madaktari 8,000 wanasambazwa kwenye hospitali mbalimbali za mikoa na wilaya ili kutatua changamoto za afya na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.[​IMG]
Katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka watendaji wa Idara ya Uhamiaji kufanya misako kwenye nyumba za wageni na kudhibiti wageni wanaoingia kwenye mipaka mbalimbali nchini kutokana na kushamiri kwa wahamiaji haramu.

Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara na taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Wilaya ya Arusha.

Ukosefu wa dawa.
Akizungumzia upatikanaji wa dawa, Majaliwa alisema serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa za aina mbalimbali ili kuondoa upungufu wa dawa kwenye hospitali nchini.

Akieleza namna serikali ilivyo na nia ya dhati ya kumaliza tatizo la dawa nchini, Majaliwa alisema; “Awali tulitoa Sh bilioni 40 kwa ajili ya dawa na sasa tumeongeza fedha hadi kufikia shilingi trilioni moja.

“Tunataka kero ya upungufu wa dawa hospitalini iishe. Naagiza kila hospitali kuhakikisha inakuwa na dirisha la huduma za bure kwa wazee pamoja na duka la dawa,” alisema.


Chanzo: ITV

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!