Sunday, 7 June 2015

WANAOTAKA RAIS DIKTETA "WASHINDWE NA WALEGEE"

Kuna hadithi kuhusu familia moja masikini iliyosikia sauti ya Mungu ikisema: “Ombeni leo mambo matatu mnayotaka niwafanyie ili maisha yenu ya sasa yabadilike.”

Walijadiliana namna ya kuomba na nini waombe. Kabla hawajakubaliana, ghafla mwanamke akatafunwa na “umimi” akaomba awe na mamlaka zaidi ili asikilizwe. Kwa Mungu hilo likawa ombi namba moja.
Halafu, akaomba Mungu mumewe awe mjingamjinga ili atakapoomba utajiri anufaike yeye na watoto. Loo, hilo nalo likawa ombi namba mbili na kuthibitisha kwamba lilipokewa, ghafla familia ikashangaa “Mzee wa Kaya” akigeuka zezeta.
Mke alifadhaika kuona mumewe amekuwa vile, haraka akaomba amrudishe mumewe kuwa wa kawaida; ikawa hivyo, na hilo likawa ombi la tatu na la mwisho. Eeh bwana, jamaa walipigana! Walitwangana! Wakasambaratishana kutokana na maombi yasiyo na tija kuwapotezea fursa ya utajiri, amani na upendo. Walibaki masikini na wakaachana.
Mungu Mwenyezi anawapenda Watanzania. Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa viongozi, amewapa fursa ya kuomba: “Rais ajaye awe wa namna gani?” Sawali fupi na rahisi.
Hapa Watanzania wanatakiwa kuorodhesha sifa za rais ajaye. Lakini baadhi ya watu, waumini makanisani na misikitini, wanasiasa na watu maarufu, wapambe wa wagombea na wagombea wenyewe kutoka chama cha mungu (CCM), badala ya kuomba rais ajaye awe mwenye hofu ya Mungu, mwenye kujali haki za binadamu eti wanataka awe dikteta!
Dikteta? Hivi, wanajua ni kiongozi wa namna gani? Wanajua athari za kutawaliwa na dikteta? Nijuavyo mimi, dikteta anaua watu, ananyanyasa watu, anafuta katiba, anapendelea familia yake, anajimilikisha mali ya umma na hajali demokrasia wala haki za binadamu.
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, dikteta ni mtu anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa; mtu mwenye tabia ya kutaka lifanywe lile analotaka bila ya kupingwa. Eti rais wa aina hiyo, atakayehatarisha amani, utulivu na kusambaratisha taifa, ndiye baadhi ya wanasiasa wanaomba atawale! Najiuliza, maombi haya yakikubaliwa na Mwenyezi Mungu, tutapata lini fursa nyingine ya kumwondoa madarakani?
Wa nini rais asiyejali utawala bora, atakayefuta chaguzi akaongoza kwa mtutu wa bunduki, atakayezuia au kufuta taasisi za demokrasia kama Tume ya Uchaguzi, na Tume ya Haki za Binadamu?
Wote wamchao Mungu wakatae maombi yanayokaribisha pepo la udikteta. Watanzania waombe rais ajaye aimarishe uchumi na taasisi za demokrasia ili Watanzania waongozwe kwa haki. Pia athamini utu.
January Makamba, ambaye ni mgombea urais amewahi kusema; “Moja ya vitu vitakavyozuia rushwa ni adhabu kali ambayo itaonekana. Kwa nini madikteta wanawaua watu hadharani? Wanachojaribu kukionyesha ni kwamba kama siku moja mtu akijaribu kuwapindua atapelekwa uwanjani na kupigwa risasi hadharani. Lengo ni kuwatia watu hofu.”
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dk Anthony Diallo amewahi kusema; “Ninatamani sana rais ajaye wa awamu ya tano awe dikiteta, lakini ambaye atakuwa amechaguliwa kwa kura na wananchi, ili aje atutie adabu, kwani taifa liko katika hali mbaya, kila mmoja ni mjuaji na yote haya yamekuwa yakisababisha uvunjifu wa amani.”
Kamanda wa Polisi mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliwahi kusema; “Mimi ningetaka rais ambaye, kwa lugha yangu na gazeti lako lilishanihoji, nikasema nataka rais ambaye atakuwa dikteta kidogo.”
Watanzania wenzangu, hivi kweli baada ya miaka 54 ya uhuru tunahitaji mrithi wa Rais Jakaya Kikwete awe dikteta ndipo dawa zipatikane hospitalini; shule ziwe na walimu wenye sifa, vitabu na vifaa vya kufundishia? Kweli Watanzania wanahitaji rais dikteta ili kodi ikusanywe, polisi wakamate vibaka na mahakama zihukumu kwa haki?
Hofu yangu ni kwamba baadhi ya wagombea urais wamejiandaa kuwa madikteta. Hamjasikia aliyesema “…wapigwe tu” anataka urais? Hamjasikia wapambe wa mgombea mmoja wakisema “watake wasitake, iwe isiwe tena kwa gharama yoyote ikulu ni lazima?” Hamkumsikia jamaa aliyewaambia wanahabari “kama kuna wanaCCM hawanipendi, wahame?” Na yule aliyetumia udikteta kulazimisha Katiba Pendekezwa ndani ya Bunge Maalumu la Katiba anautaka urais.
Rais Barack Obama alipofanya ziara nchini Ghana alisema, “Afrika haihitaji viongozi imara bali taasisi imara za kuendeleza demokrasia kwa uhuru na haki.” Na alipokuja nchini alisema, “Demokrasia haipaswi kuonekana siku ya uchaguzi tu, bali katika mchakato mzima kuanzia wakati wa uandikishaji.”
Kama Obama ameliona hilo, inakuwaje 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!