Sunday, 7 June 2015

WAFANYAKAZI WA NDANI SASA KULIPWA KIMA CHA LAKI MOJA

Serikali ya Tanzania imeweka mkakati wa kuandaa muswaada utakaosaidia sekta ya huduma ya wafanyakazi wa majumbani ili kuweza kupatiwa mishahara stahiki ikiwemo kutoa muongozo na usimamizi na haki za wafanyakazi hao.



Hayo yamesemwa bungeni katika kipindi cha maswali na majibu na naibu spika wa wizara ya ajira na kazi Mh. Makongoro Mahanga ambapo amesema serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kujenga uelewa wa wadau kuhusu usimamizi wa haki za wafanyakazi hao na kuwataka waajiri kuachana na tabia ya unyanyasaji na wanaofanyiwa vitendo vya kikatili kutoa taarifa kwa taasis husika.
 
Mahanga ametaja baadhi mkataba huo ambao unasubiri kupitishwa na baraza la mawaziri ili uweze kujadiliwa bungeni kuwa ni pamoja na kujenga uelewa wa wadau kuhusu haki za wafanyakazi wa nyumbani na kufanya tafiti linganifu kuhusu sheria za kazi dhidi ya matakwa ya mkataba huo.
 
Ameongeza kuwa serikali inasikitishwa na tabia za unyanyasaji zinazofanywa na waajiri na kuwa mpaka sasa wamefanya jitihada za kukagua katika maeneo mengi ya majumbani ili kubaini unyanyasaji huo.
 
Akizungumza kuhusu kima cha chini cha mfanyakazi wa ndani Mahanga amesema mpaka sasa mfanyakazi wa ndani anatakiwa kulipwa mshahara usiopungua kiasi cha laki moja kwa mwezi.
 
Mpaka sasa wafanyakazi wa majumbani kama walivyo wafanyakazi wengine wanaendelea kulindwa na sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!