Monday, 25 November 2013

MTOTO WA MIAKA 6 ALAWITIWA, AHARIBIWA.

Stori: Joseph Ngilisho, Arusha
Dunia haina huruma! Mtoto wa kiume ambaye ni denti wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka sita anayesoma katika shule moja ya msingi iliyopo Olasiti jijini hapa, anadaiwa kulawitiwa hadi kuharibiwa vibaya sehemu za siri.
Mtoto aliyelawitiwa akiuguzwa hospitalini.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea hivi karibuni, inadaiwa kuwa kitendo hicho kilifanywa na kinyozi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50.
Akizungumza akiwa na shangazi yake  katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru alikolazwa akipatiwa matibabu, mtoto huyo alimtaja mtuhumiwa kwa jina moja la Abuu, mkazi wa eneo hilo ambaye alimrubuni mwathirika huyo kwa ofa ya kumnyoa nywele.
Alidai Abuu amekuwa akimfanyia mchezo huo mchafu majira ya mchana au usiku katika nyumba ambayo haijamalizika kujengwa (pagale) na wakati mwingine humzungusha nyuma ya saluni yake.


Akiendelea kupata matibabu hospitalini.
Ilidaiwa kuwa hali ilikuwa mbaya baada ya mtoto huyo kushindwa kutembea na kutokwa na haja kubwa bila mpangilio jambo lililomshtua shangazi yake ambaye aliachiwa mtoto huyo yatima.
Kwa mujibu wa shangazi yake, alianza kumfuatilia kwa ukaribu ili kujiridhisha na tabia aliyokuwa akiihisi ndipo siku moja baada ya kuulizia kwa watoto wenzake, alielekezwa mahali alipo mtoto huyo ambapo alikwenda katika nyumba inayojengwa na kukuta mtoto akinajisiwa laivu na Abuu.
Alisema aliipeleka ishu hiyo kwa balozi wa nyumba kumi ili hatua zaidi zichukuliwe lakini anashangaa kuona Abuu akiendelea kudunda mtaani bila hatua zozote kuchukuliwa huku yeye akiendelea kuuguza hospitalini baada ya kuripoti polisi na kupewa fomu ya matibabu (PF-3).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alipoulizwa alisema bado hajapata taarifa za tukio hilo lakini akaahidi kulifuatilia.

GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!