Monday 22 February 2021

Usonji/ Autism Ni tatizo lisilojulikana kwa wengi elimu zaidi inahitajika

 


AUTISM/USONJI. Ni changamoto ambayo inaathiri jinsi akili inavyotuma na kupokea ujumbe kwenye milango ya fahamu,ndio maana watoto wenye hiyo changamoto wengi wao hushindwa kutafuna chakula,hawapendi kelele na hawapendi kuguswa


Usonji umebeba vitu vingi ndani yake,yani changamoto mbalimbali anazokutana nazo mtoto ndo inafaamika yule ana usonji, hutokea kipindi Cha ukuaji wa mtoto na ukitaka kugundua tatizo ni lazima mzazi kuwa karibu na mtoto na kufuata mwenendo wa ukuaji wake!Hivyo basi dalili za kutaka kugundua uyu mtoto ana usonji huwa zinaanza kuonekana mtoto akiwa na miaka mitatu(3) 

hizi ni baadhi ya dalili:

1;Mtoto upenda kujitenga na watoto wengine na kuwa mnyonge. 2;Hawezi kujieleza kwa anachotaka zaidi utumia ishara au lugha ya picha. 

3;Mzito kuzungumza na anaweza rudia neno ilo ilo mara kwa mara au upenda kumuigilizia mwenzake akiongea. 

4;Kushindwa kutazama watu usoni. 

5;Utukutu. 

6;Akili yake kuwa slow katika kila unachomwambia.

  • Tabia zilizozoeleka - Kama  kupiga piga mikono, kutikisa tikisa kichwa mara kwa mara na kujibiringisha mwili
  • Tabia ambazo huchukua sana muda kama za kupanga panga vitu kwa mpangilio maalum au kuosha mikono mara kwa mara
  • Tabia ya kung’ang’ania vitu visihamishwe kwa mfano viti au kutokubali kukatizwa katizwa

Ugunduzi (Diagnosis)

Ugunduzi wa tatizo hili la usonji hufanyika kwa

  • Daktari wa watoto  (Pediatrician) kumpima vipimo vya kawaida pamoja  na kuchukua historia ya  ukuaji wa mtoto husika (Developmental milestones)
  • Daktari bingwa wa watoto aliyebobea kwenye matatizo ya kisaikolojia ya watoto (Pediatric neuropsychologists) kumpima ili kuangalia tabia za mtoto huyu  na uwezo wake wa kiakili (Cognitive skills)
  • Vipimo vya kijenitikia (genetics testing) kama high-resolution chromosome and  fragile X testing. Hufanyika baada ya   kugundulika kwamba chanzo cha  tatizo la usonji ni matatizo ya kijenetiki

Kadri mtoto anavyoendelea kukuwa ndio usonji unavyoweza kutambulika kwa urahisi zaidi kwani madhara yake yanaonekana kwa urahisi wakati wa  ukuaji wa kiakili wa mtoto.

Uchunguzi

Mchunguze mtoto wako kwa viashiria vya tatizo la usonji mapema zaidi kwani kumchelewesha mtoto mwenye usonji kupimwa na kupewa tiba mapema huchangia tatizo hili kuwa kubwa zaidi na hivyo kuathiri matokeo ya matibabu ya tatizo hili. Nusu ya wazazi hugundua watoto wao wana tabia zisizo za kawaida ndani ya miezi 18 ya umri wa mtoto, na moja ya tano ya wazazi hugundua ya kwamba watoto wao wana tabia zisizo za kawaida ndani ya kipindi cha miezi 24 ya umri wa mtoto 2.Tabia hizi ambazo si za kawaida katika ukuaji wa mtoto ni;

  • Kutotamka maneno ya kitoto (no babbling)  mpaka anapotimiza umri wa mwaka mmoja
  • Kushindwa kuotesha kidole au kumpungia (waving, gesturing etc) mzazi/mtu yoyote mkono mpaka anapotimiza umri wa miezi 12
  • Kushindwa kutamka neno lolote mpaka anapotimiza umri wa miezi 16
  • Kutotamka maneno mawili kwa pamoja au sentensi mpaka umri wa miezi 24
  • Kupoteza uwezo wa kuongea au kutokuwa na tabia ya kutangamana/kuchanganyikana na watu wengine wakati wowote ule katika umri wa mtoto

Matibabu

Familia yenye mtoto mwenye tatizo la usonji huhitaji kuelemishwa jinsi ya kuishi na mtoto huyo pamoja na kusaidiwa katika malezi yake. Kwa kuwa tatizo hili  halitibiki ni muhimu mtoto kupata:

  • Tiba ya Tabia
    • Uchambuzi wa tabia (ABA): Kutumia utaalamu wa kisaikolojia kufundishia na kuwahusisha na jamii, kuboresha mawasiliano, na usimamizi wa kitabia
    • Matibabu na elimu ya usonji kwa kuboresha mawasiliano kwa watoto wenye ulemavu (TEACCH)
  • Tiba nyingine muhimu ni kuelimisha jamii kuhusu watoto wenye usonji , jinsi ya kuishi nao na kuwaanzishia watoto wenye usonji matibabu mapema. 

 Hizo Ni baadhi tuu lakini ziko nying sana na uwa ziko tofauti tofauti kwa kila mtoto! Hivyo basi kwa mzazi au mlezi mwenye mtoto wa usonji anatakiwa kumpa upendo sana sana ili kujua ata ishara zake akiwa anahitaj kitu flani,kwa mfano kuna watoto wasoweza kuongea kuwa anahitaj kukojoa ila unakuta tuu kashakojoa ivyo mzazi/mlezi ukiwa karibu na mtoto wako ni rahis kuona ishara ambayo akitaka kukojoa huwa anafanya! 

Na pia ukishafaham mwanao ana hili tatizo, mzazi jaribu kuikubali hali na kujua jinsi gani ya kumsaidia maan sio wazazi wote hupokea positive hii changamoto na kitu kikubwa zaidi kwa mtoto chochote unachotaka kumfundisha hakikisha unafanya nae HAND TO HAND itamsaidia kuimprove kutoka sehem moja kwenda nyingine na pia watoto hawa ni wepesi kusahau hivyo haihitaji KUKATA TAMAA!

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!