Wednesday 14 November 2018

Tabia ya kawaida kwa Mtoto ni tabia gani?

Tabia ya mtoto ya kawaida inategemea na umri wa mtoto mwenyewe, maumbile yake na hisia zake jinsi zinavyokua. Tabia ya mtoto inaweza kuwa ni tatizo kama haitaendana na matarajio  ya wazazi wake, au familia yake  na hata kama tabia yake itakua n ya fujo kila mara. Tabia nzuri huwa iko katika aina za kijamii, kiutamaduni na maendeleo ya mtoto wako kwa ujumla. Wewe kama mzazi unachotakiwa kufanya ni kuwa unafahamu hasa nini mtoto wako anatakiwa kuwa na tabisa gani kwa wakati flan kulingana na jinsi anavyokua.


nini unatakiwa kufanya kubadilisha tabia ya mtoto wako.
Watoto huwa wanaendeleza tabia kama wakipewa zawadi na wakati mwingine huacha tabia kama wazazi wakiamua kuipuuzia. Jinsi  wewe unavyoichukulia tabia ya mtoto wako kila mara ni muhimu kwa sababu kumpa mtoto zawadi au kumudhibu kwa tabia ile ile huwa inamchanganya mtoto. Kama unafikiri tabi ya mtoto wako itakua ni tatizo basi una hatua tatu za kufanya.
  • Tambua kuwa tabia sio tatizo. Hii ni kwa sababu tabia zingine huwa zinakuja sababu ni wakati na umri ambao mtoto wako amefikia.
  • Jaribu kumuachisha hiyo tabia kwa kuipuuzia au kwa kumudhibu kidogo. Sasa hapa ndio hatua nyingine hufata. Kwa sababu tabia huja kwa sababu ni wakati wake kwa hiyo cha kufanya ni kuangalia kama hiyo tabia ni nzuri au ni mbaya kama ni mbaya basi mrekebishe aache.
  • Mfundishe tabia mpya ambayo uniona ndio itakua nzuri kuliko hiyo ambayo yeye ameianzisha
Jinsi gani unaweza kuzuia mtoto asiwe na dharau.
Njia nzuri ya kumzuia mtoto asiwe na dharau ni kwa kumuelezea kwa taratibu jinsi gani hiyo tabia inakuudhi. OK  kwa watoto wetu wa kiafrica huwa tunaamini eti ukimwambia tu hawezi kuelewa ila sema kweli tangia mdogo kama ukianza kumuelewesha taratibu bila maswala ya kumpiga basi atakuelewa tu. Sasa kama wewe ndio wenzangu na mie ni fimbo kwa kwenda mbele basi hamna jinsi.
Jinsi gani unaweza kumshawishi mtoto awe na tabia nzuri.
Njia nzuri ya kumshawishi mtoto awe na tabia nzuri ni kwa kumpa zawadi. Watoto ambao wanajifunza kuwa tabia mbaya sio nzuri kwa wazazi na tabia nzuri zinawafurahisha wazazi na wanapewa zawadi, basi huwa wanajifunza mambo mengi mazuri ambayo yatakuwa na manufaa kwao huko baadae. Hii huwa inafanya kazi vizuri kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka miwili, inaweza kuchukua miezi hata miwili ili mtoto aweze kuzoea, kwa hiyo hapo unahitaji kuvumilia na kufatilia tabia zake.
Chagua tabia moja au mbili ambazo unataka kuzibadilisha, kwa mfano, mda wa kulala, kuoga, kupiga mswaki, alafu baadae chagua zawadi ambayo unahisi mtoto wako ataipenda, kwa mfano kama akikubali kuoga mapema billa kukusumbua basi unamuongezea mda kulala, au kama akikubali kula chakula vizuri bila kumwaga mwaga basi unamwambia utamuachia aangalie katuni zake kesho. Hizo ni baadhi ya zawadi ambazo unaweza kumpa kama akionyesha tabia nzuri.
Watoto bahati nzuri ukiwaeleza taratibu na kwa upendo huwa wanaelewa kwa hiyo wala wewe usikimbilie kumkalipia na kuongea kwa

Unaweza kumawambia ”nikwambie kitu ukila chakula hiki na ukamaliza chote keso nakupeleka mjini” Na hapo kweli  unakuta kesho ulikua una safari ya mjini so ataona kweli akila chakula akamaliza inakua vizuri.

Njia gani ni nzuri za kumpa mtoto zawadi
Mpe Mda.
Mpe kazi mtoto afanye alafu mpe mda awe amemaliza ndani ya huo mda. Hapa ni kumpa mtoto kazi afanye alafu unamwambia akiweza kuifanya hiyo kazi ndani ya huo mda unampa zawadi. Kuamua ni mda gani utampa hiyo kazi hapo inabidi uangalie ni mda gani unaona utakua ni mzuri kwake kuifanya hiyo kazi.
Tengeneza List ya tabia.
Hii ni njia nyingine ambayo unaweza kuifanya. Hapa we kaa chini siku moja uandike tabia ambazo unaona ni nzuri alafu umeona mtoto wako amezionyesha na hii ni kwa kulingana na umri wake. Baada ya hapo kila ukiona ameonyesha tabia nzuri basi unampa zawadi.
Mda wa kukaa kimya.
Kama unavyojua watoto wakishakuwa wawili au watatu ndani ya nyumba basi kelele huwa haziishi, yaani ni kelele tangu asubuhi  wanaamka , mchana, na jioni.  Kwa sababu hiyo basi weka mda kwa watoto ambao unataka wakae kimya na kama wakiweza kukaa kimya basi unawapa zawadi. Kitu kingine huwa kuna wakati watoto wanaweza kuwa sebuleni alafu unashangaa tu wako kimya bila sababu yoyote labda wako wanachora au wapo wanafanya yao tu…….basi hapo unaweza kuwaambia ”Mh  nimefurahi jinsi mlivyotulia hivi kesho niwapikie chakula gani” alafu kesho wapikie chakula chao wanachokipenda.

Kwa Hisani ya blog ya Afya

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!