Monday 19 November 2018

Cholesterol ni nini?


Je unajua maana ya cholesterol?
Cholesterol au rehamu sio kitu kigeni sana katika masikio yako. Inawezekana umewahi kusikia lakini hujui cholesterol ni kitu gani. Soma katika makala hii fupi ili uweze kuelewa cholesterol ni nini?


Cholesterol ni nini?
Cholesterol ni aina ya mafuta inayopatikana kwenye damu na seli za binadamu. Kwa kawaida cholesterol inasafiri katika vifungu vidogo vidogo vinavyoitwa lipoproteins. Cholesterol yenyewe si mbaya kwa sababu mwili unahitaji cholesterol ili kutengeneza homoni, vitamini D na vimeng'enya chakula na pia husaidia viungo kufanya kazi vizuri. Hata hivyo kuwa na cholesterol nyingi kwenye damu inaweza kusababisha matatizo.
Kuna aina mbili za cholesterol
Aina ya kwanza inaitwa kwa lugha ya LDL ( LOW DENSITY LIPOPROTEIN). Hii ndio cholesterol mbaya. Sio cholesterol yenye afya. Aina hii ya cholesterol hurundikana katika mishipa ya damu hivyo kusababisha mishipa ya damu kuziba. Mishipa ya damu ikiziba husababisha damu kushindwa kutembea vizuri kwenda kwenye viungo vingine hasa moyo na ubongo. Hali hiyo husababisha mtu kupata kiharusi(kupooza) na shambulio la moyo. Kiwango cha mafuta haya huathiriwa na aina ya vyakula unavyokula, kurithiwa, uwezo wa ini kufanya kazi pamoja na mambo mengine.
Aina ya pili inaitwa HDL(HIGH DENSITY LIPOPROTEIN) Hii ni cholesterol nzuri. Ndio cholesterol yenye afya. Husaidia kuondoa cholesterol mbaya kwenye mwili. Hivyo kuwa na kiwango kikubwa cha aina hii ya cholesterol ni bora.
Vyakula vipi vinafaa
Vifuatavyo ni aina ya vyakula ambavyo husaidia kupunguza cholesterol mbaya kwenye mwili wako:-vyakula vyenye nyuzi nyuzi,mafuta ya mimea hasa alizeti na karanga, mafuta ya samaki, soya, matunda ( apple na zabibu), karanga, nafaka zisizo kobolewa,maharage.
Vyakula visivyofaa Epuka kutumia vyakula hivi kwa wingi:- nyama nyekundu, margarine, vyakula vilivyookwa au kukaangwa,
Fanya hivi ili kuepuka cholesterol kujaa kwenye mwili wako
Fanya mazoezi
Kula mlo bora
Epuka matumizi ya sigara na tumbaku
Kuwa na uzito sahihi -Epuka kitambi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!