Thursday 14 June 2018

Urusi Yatamba nyumbani Mashindano ya kombe la Dunia

Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Luzhniki kwa wenyeji Urusi kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 5-0 dhidi ya Saudi Arabia katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia.
Mechi hiyo ya aina yake imeshuhudiwa bao la kwanza likiwekwa kimiani mnamo dakika ya 12 na Ganzizky ambalo limeandika rekodi ya kuwa bao la kwanza katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huu.

Mabao mengine yametiwa kimiani na Cheryshev (43' minutes, 90'+1), Dzyuba (71' ) na Golovin (90'+4).

Baada ya wenyeji kuanza vizuri, mechi zingine za kesho zitakuwa ni Iran itakayowakaribisha Morocco na vilevile Ureno itakuwa inacheza dhidi ya Spain.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!