Wednesday 23 May 2018

ZANZIBAR:MAMA NA MWANA WAUAWA KIKATILI.

Image may contain: one or more people
Mama pamoja na mwanawawe wakiume wakutwa nyumbani kwao wakiwa wameshafariki huko Mtaa wa Nguruweni Jendele Unguja.


Tukio hilo limetokea mei 22/2018 majira ya saa 1:30 asubuhi ambapo walikutwa tayari wameshauwawa na watu wasiofahamika.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishna msaidizi wa Polisi mkoa wa kusini Unguja Kamanda Suleiman Hassan Suleiman amewataja marehemu hao kuwa ni Patima Abdalla Makame (27) mshirazi wa nguruweni jendele ambae alikuwa na jeraha katika paji la uso pamoja na mwanawe wa miezi mitano alietambulika kwa jina la Haji Ismail Haroun.
Aidha Kamanda Suleiman amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaini wahalifu hao na kuwataka wananchi kutoa taarifa katika vyombo vya dola pindi pale unapotokea uhalifu ili sheria ifate mkondo wake.
CHANZO: Mzanzibar Tv

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!