Saturday, 5 May 2018

"Mke wangu angefariki mngesema mengine"- Ajib


Nyota wa Klabu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Ibrahim Ajib amefanikiwa kupata mtoto wa kike baada ya mke wake kujifungua salama mchana wa leo huku akiwataka mashabiki wa soka kuacha kumlaumu bila ya sababu za msingi.Ajib amebainisha hayo kupitia timu yake na kusema anamshukuru Mungu kwa kumjali kupata mtoto huyo japo hapo awali alikuwa na hofu kubwa kutokana na hali aliyokuwa nayo mke wake huyo.
"Namshukuru Mungu ametujali kupata mtoto wa kike, hapo kabla nilikuwa na hofu kubwa kwasababu ujauzito wa mke wangu ulikuwa na matatizo mengi, kuna wakati nilikuwa na hofu kubwa juu ya maisha yake. Naumizwa na wanaonishambulia kupitia sms kuwa nimegoma kuichezea timu, sina sababu ya kufanya hivyo. Mpira ni kazi yangu", amesema Ajib.
Pamoja na hayo, Ajib ameendelea kwa kusema "nawasamehe kwa sababu wangesikia mke wangu amefariki kwa matatizo ya uzazi nadhani wangesema mengine".
Uongozi wa EATV kwa pamoja unampongeza mchezaji Ibrahim Ajib na mke wake kwa kuweza kupata mtoto wa kike.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!