Saturday 26 May 2018

Mbaroni kwa kulawiti watoto watatu

Image may contain: 1 person, closeup
Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Mohamedi Kaisi Hamisi mwenye miaka 47 mkazi wa kijiji cha Kawawa mkoani Mtwara, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za ulawiti.

Akizungumza na EATV, Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba mwanaume huyo anatuhumiwa kulawiti watoto watatu wenye miaka 13, 14 na 15, wa shule ya msingi Kawawa, walipokuwa wanatafuta Nazi kwenye minazi iliyopo vichakani baada ya kutoka shule

Kamanda Mkondya amesema kwamba baada ya kuwakuta watoto hao mtuhumiwa aliwatishia maisha kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama katika eneo la Nambonde.
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwepo baada ya mtuhumiwa kukamatwa (Nassoro Abdala Nyoya, Sharifa Hassani na Julieta Athanas) kwa masikitiko makubwa wameiomba serikali ichukue hatua kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!