Tuesday 1 May 2018

Mambo 5 yaliyovutia harusi ya Alikiba


Shamrashamra za harusi ya Alikiba zilianza Aprili 19 pale masikio na macho vilipoelekea mjini Mombasa, Kenya ambapo majira ya asubuhi ya saa 12 Ali Kiba alifunga ndoa na Amina Khaleef katika msikiti wa Ummul Kulthum.

Jioni ilifuatia sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Gavana wa wa jimbo hilo, Hassan Joho, ambaye ni rafiki wa karibu na Alikiba.
Sherehe katika familia hiyo ziliendelea kwani jijini Dar es Salaam, mdogo wa Alikiba, Abdukiba alifunga ndoa na Ruwayda Aprili 22.
Baada ya Abdu na Ali kufunga ndoa, juzi Aprili 29, sherehe ya pamoja ilifanyika ambayo kila mtu alikuwa akisubiri kwa hamu kuona tofauti na yale yaliyotokea Mombasa ukizingatia kuwa hapa ndio nyumbani kwao.
Sherehe hiyo ilifanyika katika hoteli ya nyota tano ya Serena iliyopo katikati ya Jijini la Dar es Salaam iliyoanza saa 1.30 usiku na kuhitimishwa saa 6.10 usiku.
Katika shughuli yake Serena kulikuwa na matukio mbalimbali yaliyotokea ambayo yalikuwa kivutio kwa waalikwa na wale ambao walikuwa wakifuatilia kupitia kituo cha Azam na mitandao ya kijamii.
Kuwakutanisha watu maarufu
Moja ya jambo kubwa katika sherehe hiyo ni kuwakutanisha watu mbalimbali maarufu wakiwemo viogozi, wanasiasa, wasanii na wadau wa mpira.
Wageni hao ni pamoja na Mke wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, mama Salma ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Kwa upande wa wasanii alikuwapo Mwana FA, Christian Bella, Vanessa Mdee, MimiMars, Idris Sultan, Bilnass, Esha Buheti, Ommy Dimpoz ambaye alikuwa mwanakamati na wengine wengi.
Wadau wa mpira pia hawakuwa nyuma, ambapo Haji Manara Msemaji wa timu ya Simba alinogesha sherehe hizo na wachezaji Emmanuel Okwi na Haroun Canavaro.
Watoto wa mabwana harusi kukabidhi pete za ndoa
Muda mfupi baada ya maharusi wote kuingia ndani yaukumbi, mtoto wa Kiba, Prince Samir na wa Abdu Kiba, waliitwa kwenye jukwaa walipokaa maharusi kwa ajili ya kuwakabidhi pete ili wavalishane.
Kupata ofa ya kutembelea hifadhi za Taifa
Ilipofika muda wa kutoa zawadi na kuitwa mbele Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla, alitangaza kuwapa ofa Alikiba na mkewe kwenda kutembelea Kivutio chochote cha utalii watakachoona kinawafaa katika fungate yao na kuahidi gharama zote kulipia yeye.
Kuzindua kinywaji chake
Tukio jingine kubwa lililojitokeza katika harusi hiyo ni ile ya kuzindua kinywaji chake cha kuongeza nguvu alichokipa jina la Mofaya.
Kinywaji hicho Kiba alikitambulisha baada ya waalikwa kumaliza kupata chakula cha jioni na kueleza nia yake ya kuingia katika biashara hiyo.
Kuhudhiriwa na Mawaziri watatu
Harusi ya Kiba ilipofanyika Mombasa, mmoja wa kivutio alikuwa Gavana wa Mombasa, Hassan Joho kutokana na kuwa mmoja wa watu wakubwa katika medani za kisiasa nchini Kenya.
Lakini hapa Tanzania tumeona namna gani harusi hiyo imehudhuriwa na viongozi wakubwa katika nchi akiwamo Waziri, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!