Sunday, 15 April 2018

Mmiliki wa mabasi ajipiga risasi mdomoni yatokea kisogoni

MFANYABIASHARA maarufu wa mkoani Tabora ambaye pia ni mmiliki wa mabasi ya HBS, Sultan Ahmed amejiua kwa kujipiga risasi akiwa nyumbani kwake Sikonge mkoani Tabora.


Sultan maarufu kwa jina la ‘Chapa’ mwenye asili ya Kiarabu, alifariki jana asubuhi baada ya kujipiga risasi. Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa ambaye alisema uchunguzi ili kubaini sababu zilizosababisha kifo hicho unaendelea. Alisema Sultan alikuwa anamiliki kampuni hiyo ya mabasi na kituo cha mafuta kilichopo Sikonge.
Kwamba alikutwa na umauti baada ya kujipiga risasi mdomoni na risasi kutokea kisogoni. “Bado tunachunguza tukio hilo ili kubaini sababu zilizomfanya achukue uamuzi huo wa kujiondoa uhai wake,” alisema Mtafungwa alipozungumza na gazeti hili. Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani (TABOA), Enea Mrutu, alisema wamepokea taarifa ya msiba huo kwa masikitiko makubwa, kwa kuwa marehemu alikuwa mmoja wa wanachama wa TABOA.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!