Saturday 31 March 2018

Watu wasiojulikana wamemuua Mhasibu wa Tume ya ushindani nchini (FCC) Bw.Alex Malata na kumtupa baharini eneo la daraja

FB_IMG_1522482957367.jpg
Watu wasiojulikana wamemuua Mhasibu wa Tume ya ushindani nchini (FCC) Bw.Alex Malata na kumtupa baharini eneo la daraja la Nyerere jinini Dar.


Alex alipigiwa simu juzi akiwa nyumbani kwake Gongo la Mboto na mtu ambaye bado hajatambulika akitaka waonane katika daraja la Nyerere maarufu kama daraja la Kigamboni. Inadaiwa Alex alipanda daladala lakini mtu huyo akawa anamsisitiza ajitahidi kuwahi, hivyo aliamua kukodi bodaboda ili awahi.

Alipofika darajani Alex alimwambia dereva wa bodaboda amsubiri, kuwa kuna mtu anaenda kuongea naye (upande wa Kigamboni). Dereva alimsubiri kwa muda bila mafanikio, akampigia simu lakini hakupatikana. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu akaamua kuondoka.

Alex hakuonekana tena kuanzia wakati huo, hadi jana jioni mwili wake ulipookotwa ufukweni mwa bahari ya Hindi karibu na daraja hilo la Kigamboni. Alex ni mhitimu wa Chuo kikuu cha Dodoma (Shahada ya kwanza), na Chuo Kikuu Mzumbe (Shahada ya Uzamili). R.I.P Alex.!


JMF.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!