Wednesday, 28 March 2018

Diamond aombwa kuwa Balozi wa Maadili

Image result for diamond platnumz
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ anafaa kuwa balozi wa maadili kutokana na ushawishi mkubwa alionao.


Waziri Mwakyembe ameyasema hayo baada ya kumalizika kwa kikao kujadili sintofahamu iliyotokea baada ya baadhi ya nyimbo za msanii huyo kufungiwa.
“Ndio balozi wetu, balozi wa maadili pia, kwa sababu Diamond utake usitake yeye ni balozi wa Tanzania kwa kila kitu na safari hii tumemuomba hata maadili awe balozi wetu," amesema Mwakyembe.
Amesema, uamuzi wa kuzifungia baadhi ya nyimbo yanafanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa kiongozi wa wizara.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juliana Shonza amesema, suala la kulinda maadili ni endelevu na wakati umefika sasa kwa Bodi ya Filamu na TCRA kukamilisha zoezi la kuoanisha kanuni za madaraja ya kazi za sanaa ili kazi zinazofaa kuonekana na watu wazima zianze kuangaliwa saa sita usiku hadi saa 12 asubuhi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!