Tuesday 20 February 2018

Walimu waonywa nguo za kubana

TUME ya Utumishi ya Walimu imeonya walimu na kuwataka kuacha kuvaa nguo za kubana ambazo zinaleta ushawishi kwa wanafunzi na kusababisha kuwadharau.


Tume hiyo pia imewataka walimu waache kuvaa fulana zenye maandishi ya ajabu ili kuwapa mwanya wanafunzi kuzingatia wanayosoma wakiwa darasani.
Katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu Taifa, Winifrida Rutaindurwa ametoa onyo hilo wakati anazungumza na walimu kuhusu utendaji kazi wao wa kila siku.
"Unakuta mwalimu anaingia darasani kufundisha akiwa amevaa fulana iliyoandikwa Don't follow me (usinifuate) au swallow me (Nimeze), ambazo ukiingia darasani lazima mwanafunzi akushangae kwa kutafsiri fulana uliyovaa, badala ya kusikiliza kile unachofundisha," amesema na kuongeza:
"Acheni kuvaa nguo za kubana ambazo zinaleta ushawishi mkubwa kwa wanafunzi na kufanya kuwadharau walimu kutokana na matendo yenu".
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi Wilaya ya Chamwino, Khalid Shaban amesema, wilaya ya Chamwino imeshika nafasi ya pili kimkoa katika ufaulu wa matokeo ya mwaka huu, kitendo ambacho kinadhihirisha wanachapa kazi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!