Wednesday 21 February 2018

Serikali Yaridhia Gharama za Mazishi ya Akwilina ya Mil 80 Kwa Masharti

Familia ya marehemu Akwilina Akwiline inaendelea na maandalizi ya mazishi, huku ikielezwa kuwa Serikali imekubali kuyagharimia lakini si kutoa fedha.

Serikali imefikia hatua hiyo baada ya jana Februari 20,2018 familia ya Akwilina kueleza kuwa bajeti ya mazishi ni Sh80 milioni.
Katibu wa kamati ya mazishi Moi Kiyeyeu, ambaye ni kaka wa Akwilina amesema Serikali imewajibu kuwa haitawapa fedha taslim bali itagharimia vitu vilioorodheshwa katika bajeti ya mazishi hayo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!