Saturday 24 February 2018

Mbongo adakwa na dawa za kulevya, ahukumiwa

Mwanamke raia wa Tanzania Basaida Zena Jaffary 
amehukumiwa miaka 5 jela baada ya kukamatwa 
akiwa na mzigo wa dawa za kulevya Kilogram 2.3, 
aina ya Cocaine na Heroine, zinazokadiriwa 
kuwa na thamani zaidi ya Milioni 155.


Bi. Zena Jafary ambaye ni mfanyabiashara wa chakula aliwasili nchini Ghana katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka akitumia Ndege ya Shirika la Rwanda Air
Maafisa wa Mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya nchini humo walibaini shehena hiyo ya dawa hizo haramu zilizowekwa katika bahasha mbili
Baada ya kuhojiwa na maafisa hao, Bi. Zena alikiri kumiliki bahasha hizo na kwamba, alipewa Bw. Mandanje Omari raia wa Tanzania na kutakiwa kuzifikisha kwa mtu mmoja anayeishi katika Jiji la Accra.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!