Monday 18 September 2017

Kortini kwa kujifanya mwanamke ili aolewa

KIJANA aliyetambulika kwa jina la Sharifu Issah maarufu kama Zamda Salumu mkazi wa Manispaa ya Mtwara amefi kishwa mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa kujifanya mwanamke na kumshawishi mwanamume mwenzake kufunga ndoa.


Akisoma kesi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Hakimu Mkuu Mkazi Richard Kabate alisema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 157 cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kabate alidai kuwa mshtakiwa kati ya mwezi Machi na Juni mwaka huu akiwa katika vijiji vya Mkahala na Mpanyani halmashauri ya Nanyamba mkoa wa Mtwara kwa makusudi alijifanya mwanamke na kumshawishi Mustapha Saidi Nurdini kwa kumtongoza na kufunga naye ndoa isiyo halali.
Hata hivyo, Hakimu Kabete alisema kitendo hicho kinatoa tafsiri ya ukiukwaji mkubwa wa maadili kwa watu wa jinsia moja kuishi kinyumba. Mshtakiwa aliposomewa shitaka hilo na wakili wa serikali George Makasi, alikana shitaka hilo na upelelezi wa kesi hiyo unaendelea huku mshtakiwa akiwa amerudishwa mahabusu na kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo Septemba 28, mwaka huu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!