Tuesday, 8 August 2017

Wananchi wawafukuza Tanesco Kimara


Wananchi wamewatimua wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) waliokuwa wakikata umeme kwenye nyumba zilizopo eneo la Kimara Stop Over jijini hapa, zinazotakiwa kubomolewa ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro- Dar es Salaam.


Tayari shirika hilo limeshakata umeme kwenye eneo la Mbezi Kibanda cha mkaa na hivyo kuwalazimisha baadhi ya wenye nyumba kufungasha mizigo na kubomoa nyumba zao kwa hiari.
Hali ya huzuni na simanzi ndiyo ambayo imetawala kwenye maeneo ambako wananchi watakumbwa na bomoabomoa huku wengi wakilalamikia sheria ya mita 121.5 badala ya ile ya awali ya 60

Mwananchi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!