Friday 4 August 2017

KISUTU: YALIYOJIRI KESI YA MANJI YA UHUJUMU UCHUMI

Yusuf Manji (kushoto) akifikishwa mahakamani.
KESI inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji na wenzake watatu imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jiji Dar hadi Agosti 9 mwaka huu kutokana na mtuhumiwa kutofika mahakamani hapo.



Watuhumiwa wenzake wakitolewa Mahakamani leo.
Kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu, Huruma Shaidi ilikuwa isikilizwe leo lakini Manji hakufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa na mawakili wake kuwa ana kesi nyingine leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Wakishuka ngazi mahakamani hapo.

Julai 5 mwaka huu, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Manji alisomewa mashtaka saba na watuhumiwa wenzake, yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogweplate number mbili za magari ya serikali jambo ambalo nalo ni kinyume cha sheria.
Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja na wote wamerudishwa rumande.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!