Saturday, 15 July 2017

Wabakaji kunyimwa dhamana


OFISI ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Makosa ya jinai Zanzibar, imesema itaendelea kushikilia msimamo wake kuzishawishi mahakama kuwanyima dhamana watu wanaotuhumiwa kufanya makosa ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji.


Mkurugenzi wa Mashtaka na Makosa ya jinai (DPP), Ibrahim Mzee alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa taarifa ya usikilizaji wa kesi za udhalilishaji wa kijinsia kwa haraka katika Mahakama zote za Unguja na Pemba.
Alisema kosa la udhalilishaji wa kijinsia linapata dhamana, lakini Ofi si DPP imesema itazishawishi mahakama kuwanyima dhamana watuhumiwa wa makosa ya ubakaji wanaofi kishwa mbele ya mahakama.
“Kuwanyima dhamana watuhumiwa wa makosa ya jinai hakumaanishi tunakiuka haki za binadamu kwa watuhumiwa... hata hizi kesi zilizosikilizwa juzi 55 wapo watuhumiwa waliopewa dhamana baada ya kukidhi vigezo inavyotakiwa mbele ya mahakama,” alisema.
Makosa yasiyo na dhamana kwa mujibu wa sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ni kesi ya uhaini, mauaji, dawa za kulevya, kukutwa na silaha pamoja na wizi wa kutumia nguvu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!