Thursday, 27 July 2017

TAARIFA KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Mwenye picha katika kitambulisho hapo juu ni Bi. Loveness Herman (69), Mbelgiji mwenye asili ya Tanzania ambaye alifariki huko Liege, Ubelgiji tokea tarehe 18 Mei 2017

Marehemu Loveness Herman kabla ya kuhamia Ubelgiji na kuchukuwa uraia wa nchi hiyo katika miaka ya 1980 alikuwa akiishi Dar es Salaam. Tokea alipohamia Ubelgiji, Marehemu alikuwa akiishi peke yake na hakuwahi kupata mtoto. 

Kwa taarifa hii, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wake wa Brussels inawatafuta ndugu zake ili wape taarifa kamili za msiba huo

Kwa maelezo zaidi piga simu katika namba hii +3226406500 au barua pepe brussels@nje.go.tz. 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!