Thursday, 20 July 2017

Majaliwa aongoza wananchi wa Mbeya kumzika Linah Mwakyembe

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wakazi wa Kyela hususani wa Kijiji cha Ikolo mkoani Mbeya katika mazishi ya Linah Mwakyembe ambaye ni Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.


Linah alifariki Julai 15 mwaka huu katika Hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akitibiwa maradhi ya Saratani ya matiti na kuzikwa jana kijijini kwao Ikolo, Kyela mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Majaliwa, aliambatana na mkewe, Mary Majaliwa,lakini pia katika mazishi hayo walihudhuria, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa, wakuu wa idara mbalimbali za chama na serikali.
Spika wa Bunge, Job Ndugai na Naibu wake Dk. Tulia Ackson pia ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo. Waziri Mkuu Mstaafu, John Samwel Malekela na Mkewe, Anne Kilango Malecela pia walihudhuria mazishi hayo yaliyomalizika muda si mrefu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!