Friday, 14 July 2017

Everton watwaa ubingwa ardhi ya Tanzania


EVERTON ya Ligi Kuu England imetwaa kombe la SportPesa katika ardhi ya Tanzania baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya 2-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Alhamisi.


Pamoja na ubingwa huo, nyota wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, ndiye aliyekuwa gumzo ndani na nje ya dimba baada ya kufunga goli kwa mkwaju wa mbali katika dakika ya 34 ya mchezo baada ya kubanwa vilivyo kwa muda mrefu na walinzi wa Gor Mahia.
Hata hivyo goli hilo lilidumu dakika tatu tu kwani dakika ya 37, Jacques Tuyisende aliisawazishia Gor Mahia kwa kichwa baada ya mabeki wa Everton kushindwa kuokoa kona na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu hiyo ya England ikitaka bao la pili kwa udi na uvumba lakini mashutu yao yaligonga mwamba huku mengine yakiokolewa na mabeki wa Gor Mahia.
Hata hivyo, Dowel Davies aliiandikia Everton goli la pili katika dakika ya 81 baada ya kufunga mkwaju mkali uliomshinda golikipa wa Gor Mahia na kuifanya timu hiyo ya EPL kuweka historia ya kuchukua kombe hilo hapa nchini.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!