Saturday 24 June 2017

Mabinti 8 wa mfalme wa UAE wapatikana na hatia ya unyanyasaji

Wana wa mfalme wa UAE wapatikana na hatia ya unyanyasajiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWana wa mfalme wa UAE wapatikana na hatia ya unyanyasaji
Mabinti wanane wa mfalme wa milki za kiarabu UAE wamepatikana na hatia ya ulanguzi wa binadamu mbali na kuwadhalilisha wafanyikazi wao na mahakama moja mjini Brussels.


Walipewa kifungo cha miezi 15 jela na kuagizwa kulipa Yuro 165,000 kila mmojawao.
Walituhumiwa kwa kuwazuia wafanyikazi 20 waliowaleta katika miliki hizo mwaka 2008.
Lakini walipatikana na hatia ya shtaka kuu la kuwatesa wafanyikazi hao.
Wanawafalme hao walikana mashtaka hayo.
Wakili wao Stephen Monod alisema alifurahi kuona kwamba idara ya haki ya Ubelgiji ilichunguza kesi hiyo ambayo imezua hisia tofauti kwa kipindi cha miaka 10 
Hakuweza kuthibitisha iwapo wateja wake watalipa faini hiyo ,akusema walikuwa bado hawajaamua kukata rufaa.
Sheikha Hamda al-Nahyan na wasichana wake saba hawakuhudhuria wakati hukumu hiyo ilipokuwa ikitolewa na wanaharakti wa haki za kibinaadamu wanasema kuwa haijulikani iwapo UAE itawapeleka nchini Ubelgiji iwapo wangefungwa.
Kesi hiyo ilibainika baada ya mfanyikazi mmoja kutoroka katika hoteli ambayo wanawafalme hao walikuwa wamekodisha nyumba za hadhi ya juu.
Walisema kuwa walilazimishwa kuwepo katika nyumba hizo saa 44 kila siku, wakilala katika sakafu, hawakupewa siku ya kupumzika, walizuiwa kutotoka katika hoteli hiyo na kulazimishwa kula vyakula vinavyowachwa na wanawafalme hao.
BBC

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!