Wednesday, 21 June 2017

Askari wa Usalama Barabarani auawa kwa kupigwa risasi Kibiti

Image result for gun
Muda mfupi uliopita askari polisi wawili wa kikosi cha usalama Barabarani Bungu, Kibiti wamepigwa risasi na kufa papo hapo wakiwa kazini eneo kati ya Bungu na Jaribu! Walikuwa watatu, mmoja wa kike kasalimika!Watu wasiojulikana wamemuua askari wa Usalama Barabarani katika Kijiji cha Bungu B wilayani Kibiti, mchana huu.

Taarifa za kuaminika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa gari la askari hao pia limechomwa moto na kwa sasa vikosi vya ulinzi na usalama vinaelekea eneo la tukio.

Tutaendelea kukujuza jina la askari huyo na namna mauaji hayo yalivyotokea hivi punde.

Chanzo: Mwananchi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!