Thursday 25 May 2017

Watanzania wako salama Uingereza

BALOZI wa Tanzania nchini Uingereza, Dk Asha-Rose Migiro (pichani) amesema hakuna Mtanzania yeyote aliyeuawa wala kujeruhiwa katika shambulio la bomu la Manchester, Arena nchini humo lililosababisha vifo vya watu 22 na kujeruhi wengine 60. 


Dk Migiro aliliambia gazeti hili kwa simu kuwa, mpaka jana mchana hakukuwa na taarifa za Mtanzania kufa au kujeruhiwa katika shambulio hilo na kwamba ikiwa kutatokea taarifa, wataujulisha umma wa Watanzania.
Awali, Polisi katika mji huo ilieleza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini kama tukio hilo la juzi lina uhusiano na ugaidi ingawa Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May alilihusisha na ugaidi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!