Sunday 28 May 2017

Jonas Mkude na mashabiki wa Simba wapata ajali, shabiki mmoja afariki


Gari walilokuwa wakisafiria baadhi ya wachezaji na mashabiki wa klabu ya Simba akiwemo nahodha wa kalabu hiyo Jonas Mkude limepinduka maeneo ya Dumila mkoani Morogoro
baada ya tairi ya gari ya nyuma kupasuka. 
walipokuwa njiani kutokea Dodoma


Shabiki mmoja mwanamke aliyejulikana kwa jina la Shose amefariki baada ya kupata majeraha makubwa. Jonas Mkude alipata majeraha madogo sana na yupo salama, majeruhi wengine wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo wamewahishwa kwenye hospital ya Morogoro.
Jonas mkude na wachezaji wengine waliokiwa kwenye gari lingine walikuwa wanaiwahi kambi ya timu ya Taifa.

Klabu ya Simba inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki no wapenzi wote wa klabu ya Simba. 

Klabu ya Simba inaendelea kuwasiliana na ndugu wa marehemu kwa ajili ya kushirikiana katika msiba mzito kwa klabu nzima ya Simba kwa kumpoteza Shabiki wake mkubwa ambaye alikuja Dodoma kuisapoti timu yake pendwa ya Simba katika kuchukua ubingwa. 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!