Wednesday 29 March 2017

Mauaji ya kinyama yatikisa Mbozi'



Image result for kijiji cha mbozi
Kwa kiasi kikubwa, mauaji hayo yanatokana na kuwapo kwa imani za kishirikina kwa baadhi ya watu kufanya hivyo kwa matumaini ya kupata mafanikio baada ya kupigiwa ramli na waganga wa vienyeji.



Kutokana na kasi hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo, amekemea vikali na kuwataka wananchi kuachana na tabia hiyo badala yake wajikite katika shughuli za uzalishaji mali na kujiletea maendeleo.
Palingo, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, alisema alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Ipapa kuwa vitendo hivyo vimeipa sifa mbaya wilaya hiyo katika jamii. Palingo alifika kijijini hapo kuzungumza na wananchi ili kujua kero zinazowakabili.
Alisema vitendo vya ukatili na mauaji vimekithiri katika wilaya ya Mbozi hali iliyosababisha mkoa wa Songwe kushika nafasi ya pili kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu, ikiwamo kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Mkuu wa wilaya alisema baadhi ya watu wamekuwa wakienda kwa waganga wa kienyeji kupiga ramli ambazo ni chonganishi, huku wakiambiwa wakafanye mauaji ya watu na kuchukua baadhi ya viungo vya miili kwa imani ya kupata utajiri, kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa.
Aidha, aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi uhalifu unapotokea ili wahusika wakamatwe kwa kuwa bila kufanya hivyo, jeshi haliwezi kujua wahalifu ni kina nani, hivyo kusababisha vitendo hivyo kuendelea kushika kasi.
Kutokana na agizo la mkuu wa wilaya, mkazi wa kijiji hicho, Julius Mwampashe, alisema wako tayari kutoa ushilikiano kwa kamati ya ulinzi pindi uhalifu utakapotokea kwa sharti la kutowataja.
Mwampashe alisema kumekuwa na ugumu kwa baadhi ya wananchi kutoa ushirikiano hasa kwa jeshi la polisi kutokana na kuwataja watoa taarifa na kusababisha maisha yao kuwa hatarini.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!