Monday, 30 January 2017

Zaidi ya watu milioni moja wasaini barua kumzuia Trump kuzuru Uingereza

Waziri Mkuu Teresa May alitangaza muwaliko huo wakati akiwa ziarani Marekani.
Haki miliki ya pichaPA
Image captionWaziri Mkuu Teresa May alitangaza muwaliko huo wakati akiwa ziarani Marekani.
Zaidi ya watu milioni moja wa Uingereza wamesaini barua ya kutoa shinikizo kwa serikali ya Uingereza kusitisha ziara rasmi iliopangwa baadaye mwaka huu ya rais Donald Trump.

Barua hiyo iliyoandikwa kufuatia agizo la rais Trump dhidi ya wahamiaji, inaeleza kuwa kuja kwake kutamuaibisha Malkia Elizabeth.
Idadi ya watu wanaoendelea kusaini kupinga Mwaliko wa Trump nchini Uingereza inaendelea kuongezeka, tangu Marekani kuweka vikwazo dhidi ya wageni hatua iliyozua ghadhabu kote duniani. 
Waziri Mkuu Teresa May alitangaza muwaliko huo wakati akiwa ziarani Marekani.
Afisi yake imesema japo haikubaliani na baadhi ya sera za Trump hata hivyo ni vyema Uingereza kuwa na ushirikiano wa karibu na Marekani.
Kiongozi wa Upinzani Jeremy Corbyin ametaka Waziri Mkuu kuahirisha ziara hiyo.
Maandamano zaidi kumpiga Trump yanatarajiwaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionMaandamano zaidi kumpiga Trump yanatarajiwa
Wengi wanaopinga wanasema ziara ya Trump nchini Uingereza itakua aibu kwa Ufalme.
Ziara rasmi za serikali Uingereza huambatana na mualiko kutoka kwa Malikia, ambae huwapokea viongozi wawili wa nchi kila mwaka.
Aiki jana Rais Trump aliweka sheria kusitisha mpango wa kuwapokea wakimbizi na hasa kuwapiga marufuku wakimbizi wote kutoka Syria na wengine kutoka nchi saba zote zikiwa za kiisilamu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!