Sunday 22 January 2017

Waziri awabana polisi ongezeko la ‘mateja'

Image result for wauza unga tanzania
SERIKALI imetoa muda wa wiki moja kwa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kutoa taarifa ya utekelezaji wa Operesheni ya kuwakamata wauzaji wa dawa za kulevya, kutokana na mkoa huo kuwa moja kati ya mikoa inayoongoza nchini kwa ongezeko la watumiaji dawa hizo maarufu kama mateja.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alitoa agizo hilo jana alipotembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya na kuzungumza na maofisa wa jeshi hilo.
Masauni alisema mkoa wa Mbeya umekuwa na ongezeko kubwa la ‘mateja’ siku za hivi karibuni, hatua inayodhihirisha kuwa jitihaza za kutosha kudhibiti uuzaji wa dawa hizo haujafanywa ipasavyo na vyombo husika.
“Haiwezekani mateja wakaongezeka na mnasema mmefanikiwa kuwakamata halafu wauzaji na wasambazaji hawajulikani walipo! Kwa nini hao watumiaji wasiwataje wanaowauzia?.Au na ninyi ni miongoni mwao?”alihoji Masauni.
Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Mbeya Benjamini Kuzaga alijibu :
“Tumejitahdi kuwatafuta lakini wengi wanaonekana kukimbia. Tuna changamoto kubwa na uwepo wa nchi jirani.
Mara nyingi tunapofanya Operesheni wanakimbilia nje ya nchi”.
Hata hivyo Naibu Waziri alionekana kutoridhishwa na majibu hayo na kuwataka polisi kuongeza kasi ya operesheni ya kuwasaka wauza unga huku pia akitaka ndani ya wiki mbili apewe taarifa ya utekelezaji wa agizo lake.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!