Monday 16 January 2017

Wanaotoa dawa bila sifa waonywa


Dar es Salaam. Msajili wa Baraza la Famasia nchini, Elizabeth Shekalaghe amewaonya wanaotoa dawa kwa wagonjwa bila ya kuwa na sifa ya taaluma hiyo kuwa siku zao zinahesabika.

Shekalaghe ametoa onyo hilo jana wakati akiwaapisha mafamasia wapya 61 ambao wanatakiwa kuanza kazi baada ya kuhitimu shahada ya taaluma ya famasia.
“Nikiri baraza imekumbwa na wimbi kubwa la watoa dawa ambao hawana sifa zinazotakiwa na wanafanya kazi hii kwa udanganyifu huku wengine wakiwa na vyeti feki, nasema waache mara moja kwani siku zao zinahesabika,” amesema.

MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!