Friday, 27 January 2017

TOKA KWA DINA MARIOS!


1.Kila siku ni siku ya kujifunza jambo jipya iwe kwa kusikia,kuona au kupitia katika maisha ya wengine
2.Jifunze Kuheshimu wengine na na wewe utaheshimika.


3.Acha uoga,wengi wetu tuna uoga wa kufanya jambo fulani.Mfano kusimama na kuongea mbele za watu,kujaribu kuanzisha biashara mpya na mengine.Pambana na huo uoga pengine unakunyima nafasi ya kukua katika kujiamini.
4.Jipende mwenyewe kwanza kabla ya kupenda wengine.Huwezi kupenda wengine wakati ndani yako huna upendo wowote.Na usidhani kujipenda wewe ni kwa kwenda saloon kushonea weaving au kujipodoa au kuvaa nguo mpya nzuri nzuri.Kujipenda kwa kukaa bar kuagiza bia na nyama choma...la hasha!
5.Jifunze kuwapenda na kuwajali wengine wote wanaokuzunguka haijalishi upungufu walionao binadamu hatulingani.
6.Una mpenzi??kama ndio basi kuwa mpenzi mwenye kukidhi mahitaji ya mpenzi wako.Ikiwemo kuwa mwaminifu,mkweli,kujali,kumheshimu mwenzako.Usiwe mtu wa kupokea tuu na wewe utoee.Nikisema kupokea tu simaanishi pesa or mali.Kama mwenzio anakujali,anajitolea kwako,anakusikiliza,anakuamini,anakutiii,mwaminifu basi na wewe fanya hivyo kwake.
7.Kuwa mtu mwenye kusamehe hapa ni pagumu maana kuna watu vichefu chefu.Ila yatupasa kusamehee tusikae na vinyongo.
8.Acha kulalamika juu ya matatizo yako,yafanyie kazi.Wewe ndio wakuleta mabadiliko.
9.Tambua thamani yako.
10.Jishauri wewe mwenyewe,wakati mwingine huwa tunaomba ushauri kwa watu wengine huku tukiwa na majibu sahihi ndani ya mioyo yetu.
Dina Marios

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!