Sunday 15 January 2017

SIMULIZI /MAFUNZO.

Image result for oxygen concentrator

Mgonjwa mmoja aliyelazwa hospitalini alitembelewa na ndugu zake. Alikuwa amewekwa kwenye mashine ya oksijeni na hivyo hakuweza kuongea.

Wakati wakiwa pembezoni mwa kitanda, mgonjwa huyo alichukua kalamu na kipande cha karatasi akaandika ujumbe na kumpatia mmoja wa ndugu hao ambaye alikiweka mfuko bila kukisoma huku wakiendelea na mazungumzo.

Baada ya dakika chache, mgonjwa alifariki dunia. Ndugu yule aliingiza mkono mfukoni mwake ili kujua marehemu aliandika nini. Wajua nini kilichotokea? Kwa masikitiko ujumbe ule ulisomeka hivi:

“Tafadhali sogea pembeni kidogo, umekanyaga mpira wa oksijeni. Siwezi kupumua tena, unaniua”.

FUNZO:

Je, unaahirisha kusoma ujumbe? Je, unapuuza kupokea simu kwa sababu anayekupigia tayari wamjua? Huwenda ujumbe unaochelewa kuupokea ni muhimu kwako au kwa mtu mwingine ambaye yuko katika wakati mgumu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!