Monday, 30 January 2017

Sefue ateuliwa jopo la watu mashuhuri Afrika


Dar es Salaam. Mwanadiplomasia aliyepata kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ameteuliwa kuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika jopo la Watu Mashuhuri katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

Balozi Sefue ataungana na wajumbe wengine wapya ambao ni Profesa Ibrahim Agboola Gambari (Nigeria), Balozi Mona Omar Attia (Misri) Fatma Zohra Karadia (Algeria), Askofu Don Dinis Salomão Sengulane (Msumbiji) na Profesa Augustin Loada (Burkina Faso).
(Algeria), Askofu Don Dinis Salomão Sengulane (Msumbiji) na Profesa Augustin Loada (Burkina Faso).
Wajumbe wa zamani wanaoendelea ni Profesa Youssouf Khayal (Chad) ambaye atakuwa mwenyekiti na Brigitte Mabandla (Afrika Kusini) ambaye atakuwa makamu wake.
Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa APRM tawi la Tanzania, Rehema Twalib anayehudhuria mikutano ya Umoja wa Afrika na APRM huko Addis Ababa, Ethiopia, Balozi Sefue ameidhinishwa kwenye kikao cha juu cha wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika ambao ni wanachama wa APRM, kilichofanyika Jumamosi iliyopita.
“Haikuwa kazi rahisi kupata nafasi hii. Nchi nyingi za Afrika zilileta majina ya watu wao mashuhuri ili kuingia katika jopo hili muhimu. Balozi Sefue licha ya kuwa na utumishi uliotukuka kama mwanadiplomasia, aliungwa mkono kwa nguvu zote na Serikali,” alisema Twalib.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!