Sunday 15 January 2017

Polisi yanasa 20 kwa mauaji, shuhuda azungumza


Polisi mkoani Mara imewanasa watu 20 wanaodaiwa kumuua mkazi wa Kijiji cha Nyamatare wilayani Serengeti, Mwita Werema (35).


Werema anadaiwa kuuawa kwa madai ya kuiba mifugo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’azi amesema Werema alidaiwa kukutwa na ng’ombe wawili wanaohisiwa kuwa waliibwa katika kijiji cha jirani.
Amesema ng’ombe hao wawili ni mali ya mkazi wa Kijiji cha Kenyana Marugu Machuga (47).
Kamanda huyo amesema mauaji hayo yalitokea Januari 12, baada ya kundi la watu kumshambulia Werema kwa silaha za jadi.
Shuhuda Magesa Mangera amesema kabla ya mauaji hayo, Werema alikimbia na kujificha ndani ya nyumba ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Gwikongo, huku akiwarushia mishale waliokuwa wakimkimbiza.
Wananchi walioshiriki mauaji hayo wanadaiwa kutoka vijiji vya Kenyana, Kitunguruma, Mbalibali.
Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amepanga kuitisha mikutano kujadili wimbi la wizi wa mifugo.

MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!