Saturday 28 January 2017

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEKAMATA MAGARI MATANO AMBAYO YANASADIKIKA KUWA NIYAWIZI.


Kamishina wa Polisi wa kanda maalm ya Dar es Salaam CP Saimon Sirro akizugumza na waandishi wa habari juu ya Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limekamata magari matano ambayo yanasadikiwa kuwa yaliibiwa katika vipindi tofauti katika maeneo mblimbali jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel massaka,Globu ya jamii.




………………………………………………………………..


Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limekamata magari matano ambayo yanasadikiwa kuwa yaliibiwa katika vipindi tofauti katika maeneo mblimbali jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishina wa Polisi wa kanda maalm ya Dar es Salaam CP Saimon Sirro amesema kuwa mnamo Januari 22 mwaka huu jeshi la polisi lilikata gari aina ya Toyota karina lenye namba za usajili T950 DFN baada ya msako  wa jeshi hilo katika maeneo ya Bandari jijini Dar es salaam.
‘’Gari jingine ambalo tumelikamata Toyota Landcruseir Prado lenye namba zasajili T.959DFTgari hili katika uchunguzi wetu liliibiwa September 16 mwaka jana nabadaye kuonekana maeneo ya Mwanza januar 21 Mwakahuu’’Alisema Kamishina Simon Sirro.
Kamishna Sirro amesema kuwa jeshi hilo pia limewakamata watuhumiwa kwa wizi pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jijini  Dar es salaam na pwani pamoja na mkoa wa morogoro baada ya operesheni iliyofanywa na jeshi hilo .
Amesema kuwa jeshi hilo limewakata vinara saba wa utengenezaji wa kadi bandia za chanjo ya hona za manjano ambapo huziuza kwa watu wanaofika katika hospitali ya mnazi moja kwaajili yakupata huduma za matibabu kabla yakusafiri nje ya nchi.
‘’Baadhi yawatuhumiwa waliokamatwa nipamoja na Aisha Hassani(29)mkazi wavingunguti,Yakobo Msenga (42)mkazi wa chanika  ,Oliver Bwegege mhamasishaji (58)mkazi wa kigogo’’Ameongeza Sirro.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!