Tuesday 6 December 2016

Kifo cha Ismail wa Mbao FC, TFF yafichua siri


Ismail Mrisho Halfan (kulia) akishangilia bao lake la kwanza
 Wakati wadau wa soka nchini wakiendelea kumlilia mchezaji wa Mbao FC, Ismail Halfan aliyefariki uwanjani Mjini Bukoba juzi na kuzikwa jana Jijini Mwanza, imebainika kuwa Ismail alikuwa ni wa kwanza kuchaguliwa kuunda timu ya taifa ya vijana (U-20)


Siri hiyo imewekwa hadharani na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF alipokuwa kwenye kipindi cha 5Sports cha EATV, ambapo alisema kamati ya makocha iliyopewa jukumu la kuunda timu ya vijana chini ya miaka 20, ilimchagua mchezaji huyo mapema kabisa baada ya kuona kipaji chake kuwa si cha kawaida.

"Lengo mojawapo la mashindano yale lilikuwa ni kupata timu ya taifa ya vijana, na kwa taarifa yenu, msiba huu si wa Mbao FC pekee, ni wa taifa zima kwa kuwa mchezaji huyo alikuwa ni hazina kubwa kwa taifa, na ndiye alikuwa wa kwanza kuchaguliwa na timu ya makocha kuunda kikosi cha timu ya taifa ya vijana ambacho kingeingia kambini" Amesema Madadi.
Salum Madadi (Kulia) akiwa katika kipindi cha 5Sports. Wengine ni watangazaji wa kipindi hicho

Kufuatia tukio hilo, Madadi ameshauri kuwepo kwa magari ya wagonjwa (ambulance) yaliyokamilika katika viwanja vyote vinavyotumika kwa michezo mbalimbali ili kusaidia huduma muhimu pale linapojitokeza suala kama lililomkuta mchezaji huyo.
gari iliyotumika kumpeleka hospitali mchezaji Ismail Halfan
"Viwanja vingi vya mikoani havina ambulance, hata zikiwepo zinakuwa hazijakamilika, yaani zinakuwa hazina vifaa maalum vya huduma ya kwanza, mara nyingi ambulance zinazotumika huwa ni zile zinazomilikiwa na hospitali zilizo karibu na viwanja, ambazo nazo huwa hazipatikani kwa wakati"
Pia Madadi amevitaka vilabu kuwa na wataalam wa afya wenye uwezo na ueledi kama ambavyo kanuni za TFF kupitia kamati ya tiba zinaelekeza pamoja na kuzingatia utaratibu wa kuwapima afya wachezaji kabla ya usajili kwa faida ya klabu.
 
Ismail Halfan (kulia) mara baada ya kufunga bao
"Vilabu vingi vinadhani kuwapima afya wachezaji ni kwa faida ya wachezaji, ukweli ni kwamba kumpima afya mchezaji ni kwa faida ya klabu yenyewe ili akupe perfomance unayoitaka" Amehitimisha Madadi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!