Saturday, 12 November 2016

Askari Ajipiga Risasi Kifuani, Afariki Dunia!

askari

MTWARA: Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, aliyetambulika kwa jina la PC Sengerama amefariki dunia baada ya kudaiwa kujipiga risasi ya moto kifuani leo majira ya alfajiri wilayani Tandahimba mkoani humo.
Inadaiwa kuwa wakati askari huyo anafanya hivyo alikuwa katika lindo kwenye Benki ya NMB, Tandahimba.askari

Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari la polisi.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Henry Mwambambe amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema bado hawajafahamu chanzo cha askari huyo kujiua.
“Ni kweli kama mlivyosikia, askari huyo amefariki dunia alfajiri ya leo kwa kujipiga risasi, lakini bado hatujafahamu nini chanzo cha kujiua.
“Jeshi la Polisi linaendelea uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo, taarifa zikipatikana zenye ufasaha tutawaambia,” amesema Kamanda Mwambambe.
Taarifa zingine zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa, mwili wa marehemu umesafirishwa leo kupelekwa nyumbani kwao mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!