Sunday 1 May 2016

Orodha Ya Walioitwa Kwenye Usaili: Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere. (MJNUAT)


Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo
na Teknolojia (MJNUAT) anatarajia kuendesha usaili utakaofanyika kwa tarehe
tofauti kama ilivyonyeshwa katika tangazo hili.

Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia mambo
yafuatayo:
1. Usaili utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika kila jedwali kwenye
tangazo hili. Aidha baadhi ya kada zitakuwa na usaili wa kuandika na wa mahojiano
(written and Oral Interview), na zingine zina usaili wa mahojiano tuu.
2. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia
kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
3. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita,
Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za
mwombaji na hati zinazoonyesha ufaulu (transcripts).
4. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
7. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyia usaili.
8. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
9. Kila msailiwa awaombe wadhamini (Referees) wake aliowaweka kwenye
maombi ya kazi, kuwasilisha barua zao mapema. Hakuna msailiwa atakayeweza
kuajiriwa bila barua za marefa.Barua za marefa zitumwe kwa anwani ifwatayo:
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (MFU),
Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia, SLP 976,
Musoma.
10. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
10. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena nafasi za kazi zitakapotangazwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!